IQNA

19:57 - July 24, 2021
News ID: 3474122
TEHRAN (IQNA)- Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imelaani vikali uamuzi wa Umoja wa Afrika kuupa utawala haramu wa Israel hadi ya ‘mwangalizi’ katika taasisi hiyo ya nchi za Afrika.’

“Uamuzi huo unaupa utawala wa Israel itibari wakati unakalia ardhi zetu na pia ni fursa kwa kwa utawala huo kuendeleza mipango yake ya kufuta haki za Wapalestina na kuendeleza jinai za kinyama dhidi ya watu wetu,” imesema taarifa ya Hamas.

Taarifa hiyo imetoa wito kwa nchi za Afrika ambazo zingalia zinakumbwa na madhara ya ukolono na ubaguzi kuutumia utawala wa Israel kutoka Umoja wa Afrika na kuuwekea vikwazo.

Alhamisi Israeli ilitangaza imepata hadhi ya mwangalizi katika Umoja wa Afrika baada ya miongo miwili ya kushinikikiza kupata hadhi hiyo.

3986071

Tags: hamas ، waislamu ، afrika ، palestina ، israel
Name:
Email:
* Comment:
* captcha: