IQNA

20:41 - July 25, 2021
News ID: 3474127
TEHRAN (IQNA)-Wakati Lebanon inapambana kupitia mkwamo wake wa kisiasa uliochukua muda mrefu, Hizbullah inataka kuundwa kwa baraza la mawaziri ambalo linahudumia wananchi badala ya wanasiasa wake.

Mwenyekiti wa Baraza la Siasa la Hizbullah ya Lebanon, Sheikh Ibrahim Amine al-Sayyed alisema hayo Jumamosi, kama alivyonukuliwa na tovuti ya habari ya al-Ahed ya Lebanon.

Ni umma wa nchi yenye shida ambao unapaswa kufaidika na baraza la mawaziri kama hilo, badala ya wanasiasa wake, alibainisha.

"Hezbollah inajaribu kwa bidii kumaliza udhalilishaji na dharau dhidi ya watu, " afisa huyo alibainisha.

Uingiliaji wa kigeni na kutokubaliana kati ya kambi za kisiasa za Lebanon ni kizuizi kikuu katika kuundwa serikali ya Lebanon.

Waziri Mkuu wa mpito Saad Hariri aliwasilisha barua ya kujiuzulu kwake mapema mwezi huu baada ya kushindwa kuunda serikali.

Hariri alitaja tofauti na Rais Michel Aoun kama sababu ya uamuzi wake. Waangalizi, hata hivyo, wanataja ushawishi wa nchi kadhaa za kigeni na juhudi zao za kuiongoza Lebanon kulingana na masilahi yao kama sababu halisi mkwamo wa kisiasa nchini humo.

Weledi wa mambo wanataja Saudi Arabia ambayo inamuunga mkono Hariri pamoja na Ufaransa, dola la zamani la kikoloni ya Lebanon, na Marekani, ambayo kihistoria imekuwa ikijaribu kuona serikali iliyoko Beirut inatumikia masilahi ya utawala  haramu wa Israeli.

 Tangu mwishoni mwa mwaka 2019 na baada ya mripuko uliotokea kwenye bandari ya Beirut, Lebanon imekumbwa na mfumuko mkubwa wa bei za bidhaa na ughali wa maisha, ongezeko ambalo halijawahi kushuhudiwa la kiwango cha umasikini na mgogoro mkubwa wa kiuchumi. Hali hiyo imeshtadi kutokana na waziri mkuu Hariri kuchelewa kuunda serikali mpya katika anga iliyogubikwa na baadhi ya tofauti za kisiasa.

3475319

Tags: lebanon ، hizbullah ، serikali ، hariri ، aoun
Name:
Email:
* Comment:
* captcha: