IQNA

Kikao cha kusoma Qur'ani Tukufu kufanyika katika Msikiti wa Rey, Tehran Siku ya Ashura

12:24 - August 17, 2021
Habari ID: 3474199
TEHRAN (IQNA) - Kikao cha kusoma Qur'ani Tukufu kitafanyika Alfajiri ya Siku ya Ashura katika msikitini katika eneo la Rey mjini Tehran.

Hafla hiyo, kwa miaka 12 mfululizo kitaandaliwa kwa kuzingatia kanuni za kiafya za kuzuia kuenea kwa virusi vya corona.

Msikiti wa al-Mahdi huko Rey utaandaa hafla hiyo kwa kushirikisha idadi ndogo ya wasomaji Qur'ani Tukufu na wengine.

Imearifiwa kuwa hafla hiyo  itakuwa usomaji wa Qur'ani, hotuba na usomaji wa Dua ya Ashura.

Hafya hiyo inalenga kufufua utamaduni wa kusoma Qur'an usiku wa kuamkia Ashura na katika masaa ya mapema ya Siku Ashura kwani imesimuliwa kwamba Imam Hussein (AS) alisoma Qur'ani na dua na kusali usiku kabla ya Ashura.

Waislamu wa Shia kote ulimwenguni wanaomboleza kuuawa kwa Imam Hussein (AS), Sayyid-ul-Shuhada (bwana wa mashahidi), siku ya Ashura katika mwezi wa Muharram, mwezi wa kwanza katika kalenda ya Hijri Qamaria.

Tukio la Ashura lilijiri takribani miaka 1382 iliyopita kulingana na kalenda ya Hijria Qamaria.

Katika tukio hilo, moja kati ya vita mashuhuri katika historia ya Kiislamu na ya mwanadamu, vilitokea baina ya majeshi ya haki na batili katika ardhi ya Karbala huko Iraq. Siku hii inajulikana kwa jina la Ashura. Katika siku hiyo mjukuu wa Mtume SAW, Imam Hussein bin Ali bin Abi Twalib AS, alisimama kishujaa na wafuasi wake waaminifu 72, kukabiliana na jeshi la batili ili kuilinda dini ya Allah. Mwaka huu Ashura itasadifiana na Alhamisi, Agosti 19.

3990692

captcha