IQNA

Uvamizi wa Wazayuni katika Msikiti wa Al-Aqsa wapanda kwa 60%

22:23 - August 25, 2021
Habari ID: 3474225
TEHRAN (IQNA)-Kumekuwa na ongezeko la asilimia 60 ya idadi ya walowezi wa Kizayuni wanaouhujumi uwanja wa Msikiti wa Al-Aqsa katika mji wa Quds (Jerusalem), unaokaliwa kwa mabavu katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Palestina walowezi 9,000 wa Kizayuni wamevamia msikiti huo katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita, ikilinganishwa na 6,133 katika kipindi kama hicho mwaka jana.

Walowezi wa Kizayuni aghalabu wanavamia ua za Msikiti wa Al-Aqsa kutoka Lango la Maghariba kila siku, chini ya ulinzi wa polisi wa Israeli.

Wazayuni wao wachochezi, na pia hufanya sala za Talmud katika sehemu za mashariki zake katika uwanja wa msikiti huo.

Katika miaka ya hivi karibuni, utawala wa Kizayuni wa Israel umeshadidisha hujuma na uvamizi wake dhidi ya maeneo ya Wapalestina ukifanya njama za kufikia malengo yake haramu katika ardhi za Wapalestina.

Msikiti wa al-Aqsa ambao ni kibla cha kwanza cha Waislamu umekuwa ukiandamwa na njama mtawalia za utawala vamizi wa Israel, hatua ambazo zinakwenda sambamba na ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika maeneo ya Wapalestina.

3475570

captcha