IQNA

Israel ilikiuka haki za Wapalestina mara 3,800 Ukingo wa Magharibi, Al-Quds mwezi Julai

22:21 - August 05, 2021
Habari ID: 3474162
TEHRAN (IQNA) - Wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel na walowezi wa Kizayuni walikiuka haki za Wapalestina katika zaidi ya mara 3,800 mwezi Julai katika katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na mjini al-Quds (Jerusalem).

Ofisi ya vyombo vya habari ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) katika Ukingo wa Magharibi ilisema katika ripoti iliyotolewa Jumatano kwamba ukiukaji 3,886 ulirekodiwa mnamo Julai, pamoja na mauaji saba.

Katika ripoti hiyo ya, ofisi hiyo ilisema Wapalestina 2,140 walijeruhiwa katika visa 206 vya ufyatuaji risasi na wanajeshi wa Israeli na mashambulio 62 ya walowezi wa Kizayuni.

Kulingana na ripoti hiyo, idadi ya waliojeruhiwa iliongezeka kwa karibu asilimia 48 ikilinganishwa na Juni, wakati visa 1,449 vya kujeruhiwa vilirekodiwa.

Ripoti hiyo pia ilirekodi uvamizi wa Israeli mara 115 kwenye nyumba za Wapalestina na uvamizi 325 katika maeneo tofauti kote Ukingo wa Magharibi na al-Quds ambapo Wapalestina 406, wakiwemo wanawake na watoto, walikamatwa.

Julai pia iliona mashambulio 22 ya wanajeshi wa Israeli na walowezi kwenye maeneo ya ibada, ofisi hiyo ilisema. Zaidi ya walowezi wa Kizayuni wapatao 3,300 wa Israeli walivamia Msikiti wa al-Aqsa chini ya ulinzi kutoka kwa wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel katika kipindi hicho hicho.

Idadi ya Waisraeli katika makazi zaidi ya 230 yaliyojengwa tangu uvamizi na ukaliwaji mabavu  wa 1967 wa Ukingo wa Magharibi na al-Quds Mashariki inazidi 600,000.

Kulingana na ripoti hiyo, utawala wa Israeli uliharibu nyumba 32 za Wapalestina mnamo Julai.

Ofisi hiyo ilisema ukiukwaji mwingi uliripotiwa huko Nablus, Tubas, na al-Khalil (Hebron).

3475437

captcha