IQNA

Waafghani 200 na askari 13 wa Marekani wauawa katika hujuma Kabul

22:22 - August 26, 2021
Habari ID: 3474229
TEHRAN (IQNA)-TEHRAN (IQNA)- Raia wa Afghanistan karibu 200 wakiwemo wanajeshi 13 wa Marekani wameuawa leo kufuatia hujuma katika uwanja wa ndege wa Kabul.

Kwa mujibu wa taarifa, milipuko miwili ya bomu imejiri katika eneo ambalo kuna maelfu ya watu wamekusanyika kujaribu kuikimbia nchi kwa kutumia ndege za kimataifa tokea kundi la Taliban lidhibiti nchi hivi karibuni. Duru za hospitali mjini Kabul zinadokeza kuwa watu wasiopungua 200 wameuawa katika milipuko hiyo huku mamia ya wengine wakijeruhiwa  huku idadi ya walipoteza maisha na kujeruhiwa ikitazamiwa kuongezeka.

Msemaji wa Taliban Suhail Shaheen ametuma ujumbe kupitia Twitter na kusema: “Tunalaani vikali hujuma hii ya kinyama na  tutachukua kila hatua kuwafikisha mahakamani wahusika.”

Taliban imesisitiza kuwa hujuma hiyo imetokea katika eneo ambalo lilikuwa chini ya udhibiti wa Marekani.

Hakuna kundi lololote lililidai kuhusika na hujuma hiyo ya kigaidi.

Mataifa ya magharibi yalikuwa tayari yameonya juu ya uwezekano wa shambulio katika uwanja wa ndege wa Kabul katikati mwa juhudi za uhamishaji mkubwa wa watu. Nchi kadhaa ziliwatolea mwito raia wake kuepuka maeneo ya uwanja wa ndege, ambako maafisa walidai kulikuwa na tishio la hujuma ya kigaidi.

Tahadhari hiyo iliyotolewa siku ya Jumatano inalihusisha kundi la Afghanistan lenye mafungamano na kundi la kigaidi la ISIS au Daesh.

Jumapili tarehe 15 mwezi huu serikali ya Rais Ashraf Ghani ilisambaratika na kiongozi huyo kuikimbia nchi baada ya Taliban kuingia Kabul mji mkuu wa Afghanistan. Wachambuzi wa mambo wanasema, hatua ya wanamgambo wa Taliban ya kuudhibiti mji wa Kabul imehitimisha uvamizi wa miaka 20 wa Marekani na nchi nyingine za Magharibi kwa kisingizio cha kuijenga upya Afghanistan.Aghalabu ya viongozi na wananchi wa Afghanistan wanaamini kuwa, hali ya sasa ya nchi hiyo ni matokeo ya siasa zilizofeli za Marekani nchini humo. 

3993244

captcha