Saiyad Hussain, Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Fiji amesema Waislamu wanaoingia misikitini wanatakiwa kutumia aplikesheni ya simu za mkononi ya CareFiji.
Aidha amesema waumini wametakiwa wadumishe umbali wa mita mbili baina yao wakiwa msikitini na pia ni sharti kuvaa barakoa ili kuzuia kuenea corona.
Halikadhalika amesema wanaotaka kushiriki katika Sala ya Ijumaa wanapaswa kufika mapema msikitini ili kujisajili kwani hakuna atakayingia ndani ya msikiti bila kusajiliwa. Hussain amesema pia baada ya Sala waumini wanatakiwa kuondoka msikitini na wajiuzuie kujumuika makundi makundi.
Funguvisiwa la Fiji ni nchi iliyo kusini mwa Bahari ya Pasifiki na ina visiwa zaidi 300. Fiji ina idadi ya watu karibu milioni moja ambapo Waislamu ni karibu 60,000.