IQNA

Qur'ani Tukufu

Kozi za Qur’ani Tukufu kwa kwa walimu wa Kuwait

20:52 - October 25, 2024
Habari ID: 3479643
IQNA – Msururu wa kozi za Qur’ani zimepangwa kuandaliwa kwa ajili ya walimu wa shule nchini Kuwait. Idara ya Mafunzo ya Kiislamu ya nchi hiyo ya Kiarabu katika Ghuba ya Uajemi  itaendesha kozi hizo kwa ushirikiano na Jumuiya ya Kuwait ya Misaada na Maendeleo ya Kibinadamu.

Mafunzo hay ni kwa walimu wa shule za kiume na wa kike ambao wanaendesha mafundisho ya Kiislamu.
Abla Abdul Malik Muhammad, afisa wa idara hiyo, alisema mpango huo unalenga kuinua elimu ya Qur'ani kwa walimu na kuongeza ufanisi wa ufundishaji wao.
Kozi hizo zitafanyika mtandaoni kupitia jukwaa la Saad, ambalo linatumiwa na walimu 2,000 kote Kuwait alibainisha.
Jukwaa hilo linatoa fursa kwa walimu kuimarisha ujuzi wao wa Qur’ani, Khalid Walid al-Makimi, mwangalizi mkuu wa jukwaa alisema.
Aliongeza kuwa jukwaa hilo pia linasaidia pia katika kutathmini ufaulu wa walimu.

3490410

Habari zinazohusiana
Kishikizo: kuwait qurani tukufu
captcha