IQNA

Shughuli za Qur'ani

Tetesi za fufungwa halqa Qur'ani za Kuwait zakanushwa

20:53 - August 06, 2024
Habari ID: 3479235
IQNA - Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Kuwait ilipuuza uvumi kuhusu kufungwa halqa au vikao vya kusoma Qur'ani nchini humo.

Uvumi huo umekuwa ukisambaa katika mitandao ya kijamii katika wiki za hivi karibuni, kwa mujibu wa gazeti la Al-Watan.

Wizara hiyo imesema katika taarifa yake kwamba ina shauku kubwa ya kuona kuendelea kwa shughuli za vituo vya Qur'ani na halqa za Qur'ani katika mikoa yote ya nchi.

Hata hivyo, ilibainisha kuwa wizara inataka kukasimu baadhi ya majukumu yake na kupunguza ushiriki wake katika kuandaa shughuli hizo.

Wizara hiyo ilisisitiza haja ya kupata habari kutoka kwa vyanzo vya kuaminika na kusema kuwa itawachukulia hatua wale wanaoeneza uvumi huo wa uongo.

Shughuli za Qur'ani ni maarufu nchini Kuwait na kuna programu nyingi za Qur'ani zinazofanyika nchini humo, zikiwemo zile zinazohusisha ufundishaji wa kuhifadhi na kusoma Qur'ani.

Shughuli nyingi za Qur'ani nchini Kuwait zinatekelezwa kupitia mashirika ya kutoa misaada ya nchi hiyo.

Kuwait ni nchi ya Kiarabu yenye Waislamu wengi katika eneo la Ghuba ya Uajemi.

3489387

Kishikizo: kuwait qurani tukufu
captcha