IQNA

Diplomasia

Kundi la BRICS laidhinisha wanachama sita wapya ikiwemo Iran

18:18 - August 24, 2023
Habari ID: 3477490
TEHRAN (IQNA)- Muungano wa kiuchumi wa BRICS wa masoko yanayoibuka duniani umeamua kutoa mialiko ya uanachama kwa mataifa sita.

Hayo yamedokezwa leo Alhamisi na Rais Cyrial Ramaphosa wa Afrika Kusini ambaye ni mwenyekiti wa sasa wa BRICS.

Muungano wa BRICS - ambao kwa sasa unaundwa na Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini - unatarajiwa kuzialika Argentina, Misri, Ethiopia, Iran, Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu kujiunga.  Katika hotuba iliyochapishwa kwenye X, jukwaa la mitandao ya kijamii, ambalo hapo awali liliitwa Twitter, Ramaphopsa amesema BRICS ni kundi la mataifa mbalimbali.

Ramaphosa amesema. " BRICS Ni ushirikiano sawa wa nchi ambazo zina maoni tofauti lakini maono ya pamoja ya ulimwengu bora. Kama wanachama watano wa #BRICS, tumefikia makubaliano kuhusu kanuni elekezi, viwango, vigezo na taratibu za mchakato wa upanuzi wa #BRICS."

Rais Ebrahim Raisi wa Iran mapema leo Alhamisi aliwasili Afrika Kusini kushiriki mkutano wa kilele wa Jumuiya ya BRICS.

Nchi 23 kwa pamoja zimetuma maombi rasmi ya uanachama wa BRICS, zikiwemo sita ambazo Ramaphosa alisema zimealikwa.

Mkutano wa siku tatu wa wakuu wa nchi tano za BRICS na uwepo wa makumi ya wakuu wengine wa nchi ulianza huko Johannesburg, Afrika Kusini mnamo Jumanne, Agosti 22, 2023.

Huu ni mkutano wa 15 wa viongozi wa BRICS ambao unahudhuriwa na Rais Luiz Inacio Lula da Silva wa Brazil, Rais Xi Jinping wa China na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi. Rais Vladimir Putin wa Russia amewakilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Sergey Lavrov. Mwezi Machi, Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) ilitoa hati ya kukamatwa Putin, ambayo ilimzuia kusafiri kuhudhuria mkutano huo.

Mada kuu katika mkutano huo ni kujiunga wanachama wapya pamoja na njia za kupanua ushawishi wa kisiasa na kiuchumi wa kimataifa wa BRICS.

4164712

Habari zinazohusiana
captcha