IQNA

Sala ya kwanza ya Ijumaa katika msikiti mpya Tokyo, Japan

21:56 - September 18, 2021
Habari ID: 3474309
TEHRAN (IQNA)- Waislamu wamesali Sala ya kwanza ya Ijumaa katika msikiti mpya ambayo umejengwa katika mtaa wa Nishi Kasai eneo la Edogawa mjini Tokyo Japan.

Kwa mujibu wa taarifa siku ya Ijumaa Imamu aliwaongoza Waislamu karibu 80 katika sala msikitini hapo ambapo kuna kumbi mbili tafauti za wanaume na wanawake.

Imam Abdul Wahid amesema hii msikiti huo ambao pia una kituo cha Kiislamu utahudumi jamii ya Waislamu na pia wasiokuwa Waislamu. Amebaini kuwa watakuwa wanatoa huduma za kuuhudumia Uislamu na kufunza maadili ya Kiislamu kwa jamii nzima.

Imam Abdul Wahid amewakaribisha wote wanaotaka kujifunza Uislamu kufika katika kituo hicho huku akisisitiza kuwa,  watakuwa pia wakitoa misaada ya kijamii kwa wanaohitaji.

Naye Haroon Qureishi, Katibu Mkuu wa Wakfu wa Kiislamu Japan amesema kituo hicho kinasimamiwa na wakfu huo ambao unasimamia misikiti tisa kote Japan.

Amesema Kituo cha Kiislamu cha Nishi Kasai kimejengwa kwa ushirikiano wa Waislamu wa Japan na wafadhili kutoka nchi za 70.

Kwa upande wake,  Abdullah Baba, mwenyekiti wa Kituo cha Kiislamu cha Kasai amesema walianzisha jamii ya Waislamu eneo hilo miaka saba iliyopita ambapo kulikuwa na familia 12 hadi 15 na sasa kuna familia 80. Kwa msingi huo kituo hicho kitakuwa mchango mkubwa kwa jamii eneo hilo.

3475736/

Kishikizo: tokyo ، waislamu ، japan ، msikiti
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha