IQNA

Waislamu Japani

Misikiti Ilikuwa ni nadra kuonekana huko Japan, lakini sio hivyo tena

16:24 - May 26, 2023
Habari ID: 3477048
TEHRAN (IQNA) – Idadi ya misikiti imekuwa ikiongezeka nchini Japan katika miaka ya hivi karibuni kama vile idadi ya wafuasi wa Uislamu.

Japan sio tu nchi ya mahekalu na vihekalu ... bali pia misikiti. Hili la mwisho linatokana na kuongezeka kwa kasi kwa ndoa kati ya Waislamu na raia wa Japan na Wajapani waliosilimu zaidi ya miongo miwili ambayo imeshuhudia ongezeko la mara saba la idadi ya misikiti.

Hirofumi Tanada, profesa mstaafu wa sosholojia katika Chuo Kikuu cha Waseda huko Tokyo, anafikiri kwamba Japani sasa ni nyumbani kwa zaidi ya Waislamu 200,000.

Utafiti wa Tanada na wenzake ulionyesha kulikuwa na misikiti 113 kote Japani mnamo Machi 2021, kutoka 15 tu mnamo 1999. Idadi hiyo inatokana na takwimu za serikali na pia kwa mujibu ya idadi ya wanachama wa Jumuiya za Kiislamu Japan. Utafiti wao ulionyesha kuwa karibu Waislamu 230,000 waliita Japan nyumbani kufikia mwisho wa 2020.

Kati ya idadi hiyo, raia wa Japani na wale waliokuwa wamepata hadhi ya ukaaji wa kudumu kupitia ndoa na hali nyinginezo walichangia takriban 47,000, zaidi ya mara mbili ya makadirio ya 10,000 hadi 20,000 muongo mmoja mapema.

"Wengi wao walikua Waislamu kupitia ndoa," Tanada alisema. "Idadi inayoongezeka pia ina uwezekano wa kujiunga na imani ya hiari yao wenyewe."

Misikiti hapo zamani ilikuwa jambo la nadra sana huko Japan, lakini sio tena.

Msikiti wa hivi punde zaidi, Masjid Istiqlal Osaka, ulifunguliwa katika Wadi ya Nishinari ya Osaka mwaka jana. Msikiti hhuo uko katika jengo la zamani la kiwanda. Gharama za kazi ya ukarabati ziligharamiwa zaidi na michango kutoka kwa Waislamu Waindonesia. Indonesia inajivunia idadi kubwa zaidi ya Waislamu duniani.

Wajapani wengi hutumia msikiti huo kusali, maafisa walisema. "Tunatumai kuufanya msikiti huu kuwa sehemu ambayo Waislamu wote wanajisikia huru kusali," alisema Herizal Adhardi, raia wa Indonesia mwenye umri wa miaka 46 ambaye anaongoza chombo kinachoendesha Masjid Istiqlal Osaka.

"Sisi Wajapani hatukuwa na mazoea na Waislamu," alisema Hirofumi Okai, profesa mshiriki wa sosholojia katika Chuo Kikuu cha Kyoto Sangyo ambaye anasoma utamaduni wa Kiislamu. "Sasa kwa kuwa wao ni majirani zetu, tunahitaji kufikiria jinsi ya kuishi nao katika jamii hii yenye mseto."

3483702

Kishikizo: japan japani waislamu
captcha