IQNA

Waislamu Japan

Tokyo Camii; Msikiti mkubwa zaidi Japan

22:57 - August 09, 2022
Habari ID: 3475599
TEHRAN (IQNA)- Mtaa wa kifahari wa Yoyogi-Uehara katika wilaya ya Shibuyaj jijini Tokyo una jengo la aina yake ambalo ni msikiti mkubwa wenye rangi ya samawati.

Huu ni msikiti mkubwa zaidi Japan ambao umejengwa kwa muundo wa kipekee wa usanifu majengo wa  Uthmaniya. Msikiti huo umepewa jina la Tokyo Camii. Kwa lugha ya kituruki camii ni Msikiti. Kando ya msikiti huo ni Kituo cha Emre Yunus pamoja na duka lenye vyakula Halal na zawadi za Kiislamu.

Msikiti huo hauna chimbuko kamili la Uturuki kwani ulijengwa muongo moja baada ya kuanguka utawala wa Uthmaniya. Ulijengwa mwaka 1938 akama shule ya Kiislamu kwa ajili ya wakimbizi wa jamii za Bashkir na Tatar ambao walikuwa wametoroka Russia kufuatia Mapinduzi ya Oktoba.

Mwaka 1986, kulichukua hatua ya kubomoa jengo la mbao ambalo lilijumuisha shule na msikiti ambao ulikuwa ukijulikana kama Msikiti wa Yoyogi  kutokana na kuchakaa. Baada ya hapo serikali ya Uturuki ilifadhili kujenga msikiti ambao ujenzi wake ulimalizika mwaka 2000. Msanifu majengo wa ‘Msikiti wa Tokyo’ ni Hilmi Senalp na hivi sasa ni moja ya misikiti maridadi zaidi Asia Mashariki.

Idadi ya Waislamu wanaoishi Japan ni ndogo lakini imeongezeka katika muongo moja uliopita kutoka 110,000 mwaka 20210 hadi kufikia 230,000 mwaka 2019. Kwa ujumla kuna misikiti 110 na mashuhuri zaidi ni Tokyo Camii, Msikiti wa Okachimachi, Msikiti wa  Otsuka, Msikiti wa Nagoya na Msikiti wa Dar al Arqam.

3480030

Kishikizo: japan ، tokyo ، msikiti ، waislamu japan
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha