IQNA

Waislamu Oman wapongeza kuanza tena Sala ya Ijumaa misikitini

21:47 - September 26, 2021
Habari ID: 3474346
TEHRAN (IQNA)- Waislamu nchini Oman wamepongeza hatua ya serikali kuruhusu tena Sala ya Ijumaa misikitini baada ya kufungwa kwa muda wa miezi 18 kutokana na janga la COVID-19.

Sala ya Ijumaa katika misikiti kote Oman ilisitishwa Machi 15, 2020 kama sehemu ya hatua za kuzuia kuenea COVID-19. Amri hiyo ilibatilishwa Ijumaa 24, 2021 ambao waumini wameruhusiwa kurejea tena misikiti lakini kwa sharti kuwa idadi ya wanaosali isizidi asilimia 50 ya uwezo wa msikiti.

Idhini hiyo hiyo imetolewa kwa masharti ambapo wale tu waliopata chanjo ya COVID-19 ndio watakaoruhusiwa kushiriki katika Sala ya Ijumaa.  Aidha wanaosiriki katika Sala ya Ijumaa wanatakiwa kuzingatia kanuni za kukabiliana na COVID-19 kama vile kutokaribiana, kila moja kubeba mkeka binafsi wa kuali. Waumini wametakiwa pia watawadhe nyumbani na wajiepushe kupeana mkono au kukumbatiana.

Wizara ya Afya ya Oman  inafuatilia kwa karibu taratibu za kiafya misikitini na iwapo kesi ya COVID-19 itabainika miongoni mwa waliosalia basi msikiti utafungwa na hatua za kukabiliana na hali hiyo zitachukuliwa.

3475798

captcha