IQNA

11:50 - October 19, 2021
News ID: 3474442
TEHRAN (IQNA)- Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema chama cha Al-Quwwatul-Lubnaniyyah (Lebanese Forces) kinalenga kuibua vita vya ndani nchini humo.

Sayyid Hassan Nasrallah ameyasema hayo katika hotuba aliyotoa usiku wa kuamkia leo alipoashiria jinai iliyofanywa siku ya Alkhamisi iliyopita mjini Beirut na wanamgambo wenye mfungamano na chama cha Al-Quwwatul-Lubnaniyyah kinachoongozwa na Samir Geagea na akasema: kuna chama ndani ya Lebanon ambacho kinataka wakazi wa eneo la Dhahiyah kusini mwa Beirut wawe daima katika hali ya hofu na wasiwasi.

Katibu Mkuu wa Hizbullah amebainisha kuwa, viongozi wa chama hicho wana nia ya kuanzisha uadui bandia na kuzusha fitna kati ya Wakristo na Waislamu na akaongeza kwamba, lengo la kueneza hofu hiyo ya mtawalia ni chama hicho kutaka kionekane kuwa ndiye mtetezi hasa wa Wakristo.

Sambamba na kutoa salamu za pole kwa familia za waliouawa shahidi katika jinai ya Siku ya Alkhamisi mjini Beirut, Sayyid Hassan Nasrallah amebainisha kuwa, mapigano ya mtutu bunduki na hata kuzuka vita vya ndani hakuna umuhimu wowote kwa chama hicho cha Al-Quwwatul-Lubnaniyyah, kwa sababu kunaendana na ufanikishaji wa maslahi yake ya nje ya nchi.

Asubuhi siku ya Alkhamisi, wananchi kadhaa wa Lebanon waliokuwa wakilalamikia utendaji wa Tariq Bitar, mchunguzi mkuu wa faili la mripuko wa bandari ya Beirut waliandamana hadi mbele ya jengo la wizara ya sheria mjini Beirut, lakini ghafla wakaanza kufyatuliwa risasi na wafuasi wa chama cha Al-Quwwatul-Lubnaniyyah kinachoongozwa na Samir Jaajaa.

Raia wasiopungua saba wasio na hatia waliuawa shahidi na wengine zaidi ya 60 walijeruhiwa katika shambulio hilo.

4006205

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: