IQNA

Nasrallah: Njama za Marekani nchini Lebanon zimefeli

19:10 - August 23, 2021
Habari ID: 3474218
TEHRAN (IQNA)- Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesisitiza kuwa, kambi ya muqawama inajivunia na uadu na ubeberu wa Marekani, uadui wa utawala haramu wa Israel na mipango ya utawala huo ghasibu dhidi ya harakati hii.

Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesisitiza kuwa, kambi ya muqawama inajivunia na uadu na ubeberu wa Marekani, uadui wa utawala haramu wa Israel na mipango ya utawala huo ghasibu dhidi ya harakati hii.

Sayyid Hassan Nasrallah amesema kuwa, hatua na njama zote za ubalozi wa Marekani nchini Lebanon zimefeli na kugonga mwamba na kwamba, ubalozi huo unabeba dhima ya kulenga maisha ya wananchi wa Lebanon na umekuwa ukiingilia kila jambo.

Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, balozi za Marekani na utawala vamizi wa Saudi Arabia katika miaka ya hivi karibuni zimekuwa zikifanya njama ili kuibua vita vya ndani nchini Lebanon.

Katibu Mkuu wa Hizbullah sambamba na kuashiria kwamba, makundi yenye mrengo wa kitaifa kwa hakika yamekuwa yakitaka kuheshimiwa mamlaka ya taifa la Lebanon amesema kuwa, Marekani na wengine wametumia makumi ya mabilioni ya dola kwa ajili ya kuupaka matope muqawama lakini wamegonga mwamba katika njama zao hizo.

Sayyid Hassan Nasrallah ameongeza kuwa, awali kulianzishwa vita vya dunia dhidi ya Syria na kisha maadui hao wakatuma magaidi nchini Lebanon, lakini mipango yao hiyo michafu dhidi ya taifa hili nayo kwa mara nyingine tena ilishindwa na kugonga mwamba.

Hivi karibuni pia Nasrallah  aliashiria malengo ya vita vya kiuchumi nchini Lebanon na kusema: "Lengo la vita vya kiuchumi nchini Lebanon ni kulidhalilisha taifa na Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Lebanon (Hizbullah) ili kuliweka taifa chini ya mashinikizo na kutengeneza mazingira ya kusambaratika nchi hii.

3475557

Kishikizo: nasrallah ، lebanon ، marekani
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha