IQNA

Nasrallah: Kupambana na utawala wa Kizayuni ni kipaumbele cha harakati za muqawama

16:05 - August 19, 2021
Habari ID: 3474206
Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amehutubu kwa mnasaba wa Siku ya Ashura na kusema, 'kukabiliana na utawala wa Kizayuni ni kipaumbele cha harakati ya muqawama (mapambano ya Kiislamu)"

Akizungumza katika siku ya kukumbuka kuuawa shahidi Imam Hussein AS na wafuasi wake watiifu katika siku kama ya leo mwaka wa 61 Hijria huko Karbala, Sayyid Hassan Nasralla Katibu Mkuu wa Hizbullah ameanza hotuba yake kwa kuwatumia salamu za rambi rambi Mtume Muhammad SAW, Imam  Ali AS, Bibi Fatima Zahra SA , Imam Hassan AS na Maimamu Watoharifu AS kwa mnasaba wa siku hii.

Sayyid Hassan Nasrallah ameashiria kadhia ya Palestina na kusema: "Ashura ya Imam Hussein AS ina ujumbe huu kuwa,  watu wote wenye heshima duniani wanasimama pamoja na taifa linalodhulimiwa la Palestina."

Hassan Nasrallah ametoa wito kwa wote kusimama pamoja na taifa la Palestina katika Ukingo wa Magharibi, Ukanda wa Ghaza na pia Wapalestina wakimbizi ili taifa hilo liweze kukomboa ardhi zake zinazokaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni wa Israel. Ameongeza kuwa, 'tumeelekeza macho yetu kwa siku ambayo Wazayuni maghasibu wataondoka katika ardhi za Palestina." Ameongeza kuwa, kulinda mapambano ya Palestina si jukumu la Wapalestina pekee bali pia ni jukumu la harakati zote za muqawama.

Katibu Mkuu wa Hizbullah ameyashukuru makundi ya mapambano ya Kiislamu Iraq ambayo yametangaza kuwa tayari kufika katika medani ya mapambano ya ukombozi wa Palestina.

Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, Nasrallah amesema Marekani inaongoza madola dhalimu ambayo yanatekeleza mauaji duniani na kusema, mamlaka ya nchi za eneo pamoja na maji na mafuta ya eneo la Asia Magharibi yanapaswa kuwa mikononi mwa mataifa ya eneo mbali na satwa  na uporaji wa Marekani. Aidha ametahadharisha baada ya Marekani kushindwa Afghanistan, sasa dola hilo linataka kuendele akukalia kwa mabavu Iraq na Syria.

3991734/

captcha