IQNA

Misri yaruhusu tena darsa za kuhifadhi Qur'ani misikitini

17:31 - October 31, 2021
Habari ID: 3474496
TEHRAN (IQNA)- Wizara ya Wakfu nchini Misri imetangaza kuwa darsa za kuhifadhi Qur'ani ndani ya misikiti kwa kuhudhuria ana kwa ana waalimu na wanafunzi zitaanza tena kote katika nchi hiyo.

Darsa hizo zimefungwa kwa miezi kadhaa ili kuzuia kuenea zaidi ugonjwa wa COVID-19 ambao umeiathiri vibaya nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.

Wazri wa Wakfu Sheikh Mohamad Mokhtar Gomaa amesema darsa za kuhifadhi Qur'ani zinatazamiwa kuanza tena mapema Disemba.

Amesema suhula za kisasa zitatumika darasani kuhu wanaoshiriki wakitakiwa kuzingatia sheria za kiafya za kuzuia kuenea COVID-19. Amesema misikiti yote itatenga maeneo maalumu ya kufundisha Qur'anikwa watoto kwa sharti kuwa suhula zinazohitajika zinanunuliwa.

Algeria pia imetangaza kufungua tena vituo vya kufundisha Qur'ani ambavyo vilifungwa baada ya kuanza janga la COVID-19. Kwa mujibu wa taarifa katika msimu wa 2021-2022 kuna wanafunzu  karibu milioni moja ambayo wamejisajili kushiriki katika darsa za Qur'ani kote katika nchi hiyo.

4009317

captcha