IQNA

Kijana Mmisri mwenye ulemavu wa macho aliyehifadhi Qur’ani kwa muda wa miezi mitatu

19:54 - September 28, 2021
Habari ID: 3474352
TEHRAN (IQNA)- Abdullah Ammar Mohammad al-Sayyed ni kijana Mmisri mwenye ulemavu wa macho ambaye alifanikiwa kuhifadhi Qur’ani Tukufu katika kipindi cha miezi mitatu tu.

Abdullah anayeishi katika kijiji cha Tal al Jarad  katika jimbo la Sharqia alianza kusoma Qur’ani mwaka 2014 chini ya Ustadh Mohamad Hassan Alwan. Baada ya miezi mitatu tu alifanikiwa kuhifadhi Qur’ani Tukufu kikamilifu na baada ya hapo akaweza kuhitimu katika kusoma Qur’ani kwa mbinu 10 tafauti.

Alwan pia ana uwezo wa kufasiri aya zote za Qur’ani kwa lugha za Kifaransa na Kiingereza.

Kijana huyo ameweza kushinda mashindano kadhaa ya kimkoa, kitaifa na kimataifa ya Qur’ani Tukufu. Mwaka 2018 alifanikiwa kushinda mashindano ya kimataifa ya Qur’ani Misri.

Kijana huyo ameenziwa mara mbili na Rais Abdel Fattah el Sisi kutokana na mafanikio yake katika kuhifadhi Qur’ani Tukufu.

4000935

Kishikizo: misri qurani tukufu
captcha