
Katika sherehe hiyo iliyofanyika Jumamosi, maafisa wa ngazi za juu walishiriki akiwemo Ibrahim Hilmsi Karsli, Mkuu wa Idara ya Masuala ya Kidini katika Ofisi ya Rais.
Sherehe hiyo ilianza kwa qiraa ya Qur'ani Tukufu na kisha duaa. Akihitubu katika kikao hicho Karsli ametoa wito wa kuimarishwa ustaarabu na utamaduni wa Qur'ani kote Uturuki huku akipongeza uwepo wa idadi kubwa ya waliohifadhi Qur'ani nchini humo.
Huku akisisitiza nafasi ya Qur'ani Tukufu katika ustawi wa jamii, ameelezea matumaini yao kuwa waliohifadhi Qur'ani wataongezeka Uturuki na kote katika ulimwengu wa Kiislamu.
Katika sherehe hiyo , wanafunzi 290 waliohifadi Qur'ani walitunukiwa vyetu na zawadi.
Idara ya Masuala ya Kidini Uturuki ilitangaza kuwa mwezi Agosti watoto milioni mbili nchini humo walishiriki katika vikao vya kuhifadhi Qur'ani vilivyofanyika katika msimu wa majira ya joto kuanzia Juni 5 hadi Agosti 20 katika misikiti 61,000 na vituo 13,000 nchini humo.


