Katika ziara hiyo iliyofanyika siku ya Jumatatu, Mfalme aliangazia muundo wa msikiti huo unaolenga uendelevu wa mazingira pamoja na mchango wake mkubwa kwa jamii.
Katika taarifa iliyochapishwa na Familia ya Kifalme kwenye mtandao wa kijamii wa X, msikiti huo ulisifiwa kwa kuwa ni “wa kipekee kwa ubora wake wa usanifu majengo, uongozi katika masuala ya mazingira, na nafasi yake kama sehemu ya ibada na nguzo ya ushirikiano wa kijamii.”
Taarifa hiyo iliongeza kuwa: “Msikiti huu unaozingatia uendelevu unachanganya muundo wake na mifumo inayookoa nishati pamoja na uzalishaji wa nishati mbadala ili kupunguza kwa kiasi kikubwa uzalishaji wa hewa ukaa (carbon emissions).”
Kadhalika, Mfalme huyo alifungua rasmi Maabara Mpya ya Whittle (New Whittle Laboratory), ambayo ni kituo cha utafiti wa anga na nishati katika Chuo Kikuu cha Cambridge.
Familia ya Kifalme ilieleza kuwa maabara hiyo inashirikiana na Mpango wa Masoko Endelevu (Sustainable Markets Initiative) katika lengo la “kutafsiri uvumbuzi wa kisayansi kuwa vitendo halisi vinavyoweza kutumika duniani” kupitia ushirikiano wao.
3498352