IQNA

Muungano wa Walimu wa Marekani wataka Israel isitishe vita Lebanon na kuondolewa mzingiro kwenye bandari za Iran

15:56 - July 21, 2026
Habari ID: 3482520
IQNA – Muungano wa Walimu wa Marekani (American Federation of Teachers - AFT) umeitupia lawama utawala wa Kizayuni wa Israel kwa kusababisha mgogoro wa walimu katika ardhi za Palestina, huku ukitoa wito wa kukomeshwa kwa uchokozi dhidi ya Lebanon na kuondolewa kwa mzingiro haramu uliowekwa kwenye bandari za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Muungano huo wa walimu umesisitiza kuwa utawala wa Israel ndio unaowajibika kikamilifu kwa mgogoro wa walimu na mfumo wa elimu katika ardhi zilizokaliwa kwa mabavu za Palestina.

Katika msimamo wake thabiti, muungano huo pia umeutaka utawala wa Kizayuni “kusitisha mara moja operesheni zake za kijeshi nchini Lebanon na kukomesha mpango wa kuwalazimisha wakazi kuhama kutoka maeneo ya kusini mwa nchi hiyo.” Aidha, AFT imedai kuondolewa kwa mzingiro dhidi ya bandari za Iran, kama sharti la kuwezesha kufunguliwa kwa njia ya maji ya Lango la Hormuz.

Hivi karibuni, kura ya maoni iliyotolewa imeonesha kuwa takriban asilimia 60 ya watu wazima nchini Marekani sasa wana mtazamo hasi dhidi ya utawala wa Israel. Hii inatokana na madhara mabaya na matokeo ya vita vyake vya kikatili vinavyoendelea Gaza na uchokozi wake wa hivi karibuni dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

/3498358

Habari zinazohusiana
captcha