IQNA

Ubao adimu wa Khati ya Qur’ani ya karne ya 19 waonyeshwa katika Makumbusho ya Bahari ya Shamu

16:45 - July 18, 2026
Habari ID: 3482502
IQNA – Ubao adimu wa Khati ya Qur’ani Tukufu wa karne ya 19 unaonyeshwa katika Makumbusho ya Bahari ya Shamu (Red Sea Museum) jijini Jeddah.

Ubao huo uliotengenezwa mnamo mwaka 1859–1860 Miladi na Ghouth Mahboob Ghalib kule Mysore, India, kazi hii ya sanaa ya ukurasa mmoja inajumuisha maandishi yote ya Qur’ani Tukufu yaliyopangwa kwa ustadi ndani ya mchoro wa kina wa Msikiti Mtukufu (Masjid al-Haram) wa Makka.

Ukiandikwa kwa hati ya Diwani kwa kutumia wino mweusi na kupambwa kwa dhahabu, maandishi hayo yamepangwa huku Al-Kaaba ikiwa imewekwa katikati yake.

Khati hiyo iliyosanifiwa kwa umakini mkubwa inaanza na Surah Al-Fatihah sehemu ya juu, ikisukwa kupitia maelezo ya kiusanifu ya msikiti huo, na kuhitimishwa na Surah An-Nas.

Kitu hiki cha kale kinaangazia safari za kihistoria na kiroho za mahujaji ambao walisafiri kuvuka Bahari ya Shamu kuelekea Makka, wakiwa wamebeba kazi za sanaa ambazo zilidhibiti urithi wa utamaduni na historia tukufu ya Hijja.

3498307

captcha