IQNA

Mipaka ya Iran iko tayari kwa ajili ya wanaoelekea Ziyara ya Arbaeen

21:51 - July 20, 2026
Habari ID: 3482516
IQNA – Vituo vyote ya mipakainayoelekea nchini Iraq sasa vinafanya kazi kikamilifu na viko tayari kurahisisha uingiaji na utokaji wa wafanyaziyara wa Arbaeen, amesema afisa mmoja wa Iran.

Ali Akbar Pourjamshidian, Mkuu wa Makao Makuu ya Arbaeen, alisema siku ya Jumapili kuwa vituo vya mipakani vya Shalamcheh, Chazzabeh, Mehran, Khosravi, Bashmaq, na Tamarchin viko tayari kikamilifu kuwapokea na kuwahudumia wafanyaziyara wanaoelekea Iraq kwa ajili ya matembezi ya kiroho ya Arbaeen.

Aliongeza kuwa hakuna vizuizi vikuu vyovyote vinavyokabili safari ya wafanyaziyara hao.

“Ushauri wetu ni kwamba wananchi wachague mpaka ulio karibu nao zaidi kwa ajili ya kuondoka nchini, kulingana na maeneo walipo, ili kupunguza muda wa kusubiri mipakani.”

Pourjamshidian alitoa matamshi hayo wakati wa Kongamano la 6 la Kimataifa la Afya katika Arbaeen lililofanyika mjini Tehran.

Alibainisha kuwa hadi sasa, zaidi ya Wairani milioni moja wamejisajili rasmi ili kushiriki katika msafara wa Arbaeen wa mwaka huu.

“Utabiri wetu ni kwamba idadi ya wafanyaziyara wa Arbaeen kutoka Iran itakuwa kubwa zaidi kuliko ile ya mwaka jana,” alieleza.

Arbaeen ni maadhimisho matukufu ya kidini yanayofanywa na Waislamu, hususan wa madhehebu ya Shia, katika siku ya arubaini baada ya Siku ya Ashura, kuadhimisha kuuawa shahidi Imam Hussein (AS), mjukuu wa Mtume Muhammad (SAW) na Imam wa tatu wa Waislamu wa madhehebu a Shia.

Hii ni moja ya ziyara kubwa zaidi za kila mwaka ulimwenguni, ambapo mamilioni ya Waislamu wa Shia, pamoja na idadi kubwa ya Masunni na wafuasi wa dini nyinginezo, hutembea kwa miguu kuelekea mji mtukufu wa Karbala kutoka miji mbalimbali ya Iraq na nchi jirani. Mwaka huu, siku ya Arbaeen inasadifia tarehe 4 Agosti.

3498341

captcha