IQNA

Programu ya kuelimisha watoto kupitia Hadithi za Qur’ani katika TV ya Misri

17:04 - July 19, 2026
Habari ID: 3482507
N
IQNA – Programu ya ‘Noor’, inayorushwa kupitia Kituo cha Televisheni  cha Naas nchini Misri, iliwasilisha ujumbe wa elimu na malezi kwa mtindo rahisi kwa ajili ya watoto katika kipindi chake kipya siku ya Ijumaa.

Katika kipindi hiki, sehemu iliyopewa jina la “Hadithi kutoka katika Qur’ani Tukufu” iliwasilishwa kwa lengo la kurahisisha dhana za kidini kwa watoto. Kwa mujibu wa ripoti ya Akhbar Al-Youm, sehemu hiyo ilishughulikia hadithi ya Nabii Suleiman (AS) na dhana zinazohusiana na uchawi.

Vilevile, kipindi hicho kilielezea hatari ya kiburi na kutokushukuru neema za Mwenyezi Mungu kwa kupitia hadithi ya Qarun katika kipindi kilichopita. Qarun alikuwa mtu katika Misri ya kale ambaye alitenda dhambi na kuwa na majivuno, na hatimaye akapata adhabu ya kumezwa na ardhi.

Programu hiyo ya Kituo cha Televisheni  cha Naas iliwasilisha pia ujumbe wa kuelimisha kutoka katika “Ujumbe wa Sheikh wa Al-Azhar kwa Watoto” ambao ulisisitiza umuhimu wa kumfuata Mtume Muhammad (SAW) katika tabia na mienendo, si katika mwonekano pekee. Ujumbe huo ulinukuu aya ya 31 ya Surah Aal-Imran: “Sema: Ikiwa nyinyi mnampenda Mwenyezi Mungu, basi nifuateni mimi, Mwenyezi Mungu atakupendeni.”

Programu ya Noor ilisisitiza pia thamani za rehema, uaminifu, na unyenyekevu. Katika sehemu ya “Hadithi ya Ajira katika Enzi ya Masahaba,” ilichunguza mifano ya kazi muhimu katika kipindi cha mwanzo cha Uislamu.

Kwa kunukuu aya ya 60 ya Surah Al-Anfal, “Na waandalieni (maadui) nguvu kadiri muwezavyo,” sehemu hiyo ilisisitiza umuhimu wa kazi na uzalishaji. Ilirejelea ujuzi wa upigaji mishale na utengenezaji wa mishale wa mmoja wa Masahaba wa Mtume (SAW), pamoja na jukumu la Sahaba mwingine katika utengenezaji wa mikuki.

Sehemu hiyo ilijumuisha vipengele vya kisanaa na ubunifu kama vile “Jitengenezee Mwenyewe” na “Vipaji vya Marafiki,” pamoja na hadithi ya kusikiliza kutoka katika hadithi za Juha (mkusanyiko wa hadithi halisi za Kiarabu). Aidha, hadithi ya “Ardhi ya Zumaridi,” iliyofikisha jumbe kuhusu uaminifu, thamani ya kazi, na unyofu, ilisisitiza umuhimu wa kutumia neema ipasavyo badala ya kuzipoteza.

3498317

captcha