IQNA

Masomo ya Qur’ani ya ana kwa ana yaanzi Jakarta, Indonesia

14:04 - November 23, 2021
Habari ID: 3474592
TEHRAN (IQNA)- Kituo cha Darul Qur’an cha Jakarta, Indonesia kinachofadhiliwa na Mfawidhi wa Haram Takatifu ya Imam Hussein AS kimeanza tena masomo ya Qur’ani ya ana kwa ana.

Masomo hayo ya Qur’ani yameanza tena baada ya kusitishwa kwa muda wa miaka miwili kutokana na janga la COVID-19.

Wavulana na wasichana 250 wanatazamiwa kuhudhuria masomo hayo, amesema Mohammad Baqir Mansouri, mkuu wa kitengo cha kimataifa cha matawai la Darul.

Amesema kwa kuzingatia kupungua maambukizi ya COVID-19 katika mji huo mkuu wa Indonesia, amesema sasa mazingira yameboreka  na hivyo kuwezesha wanafunzi kushiriki ana kwa ana katika masomo.

Darul Quran Jakarta hutoa mafunzo ya kuhifadhi Qur’ani, kusoma, na tafsir.

Idara ya Darul Qur’an inayosimamiwa na Mfawidhi wa Haram Takatifu ya Imam Hussein AS hutoa masomo ya Qur’an nchini Iraq na maeneo mengine duniani.

 

4015508

Kishikizo: jakarta ، indonesia
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha