IQNA

Balozi wa Qur'ani wa Iran: Diplomasia ya Qur'ani ni Daraja Kati ya Mataifa

14:01 - March 17, 2025
Habari ID: 3480389
IQNA – Qari mashuhuri wa Iran, Hamed Shakernejad, amesisitiza umuhimu wa diplomasia ya Qur'ani, akiiita daraja kati ya mataifa.

Shakernejad alitoa maoni hayo wakati wa mkusanyiko mkubwa wa Qur'ani uliofanyika katika Msikiti wa Istiqlal ulioko Indonesia Jumapili. 

Aliongeza kuwa Qur'ani Tukufu ni msingi wa kuimarisha uelewa na maelewano kati ya mataifa, ikileta amani moyoni. 

Ahmad Abolqassemi, qari mwingine waandamizi kutoka Iran, Balozi wa Iran, na Mwambata wa Kiutamaduni wa Iran pia walihudhuria tukio la Qur'ani ambalo liliandaliwa na Waziri wa Mambo ya Kidini wa Indonesia, Nasaruddin Umar, ambaye pia ni Imamu wa Swala katika msikiti huo. 

Maqari wa Iran, pamoja na Maqari wa Indonesia akiwemo Darwin Husinwian na Mohammad Rizqan, walikariri aya za Qur'ani Tukufu, ambazo zilipokelewa kwa joto kubwa na watu wa Indonesia waliohudhuria programu hiyo.

Katika hotuba yake, waziri wa mambo ya kidini wa Indonesia aliwapongeza Waislamu kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani na kusisitiza umuhimu wa Usiku wa Nuzul al-Quran (kuteremshwa Qur'ani). 

Pia alisifu uwepo wa ujumbe wa Iran katika Msikiti wa Istiqlal huko Jakarta. 

Shirika la Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu la Iran, Mwambata wa Kiutamaduni wa Ubalozi wa Iran nchini Indonesia, na Kipindi cha Televisheni cha Mahfel walichangia katika kufanikisha programu hiyo. 

Mahfel, inayojulikana kwa kuonyesha kariri za Qur'ani na kukuza mafunzo ya Kiislamu, ni mfululizo wa televisheni wa Kiirani unaopendwa na hadhira duniani kote. 

Aidha, Mwambata wa Kiutamaduni wa Ubalozi wa Iran nchini Indonesia amepanga programu za ziada za Qur'ani katika vituo vingine kadhaa nchini Indonesia wakati wa ziara ya maqari wa Iran katika nchi hiyo ya Kusini-Mashariki mwa Asia.

3492381

captcha