IQNA

Harakati za Qur'ani

Tarjuma ya Qur’ani kwa Lugha ya Cirebon ya Indonesia

22:37 - November 01, 2024
Habari ID: 3479682
IQNA - Wizara ya masuala ya kidini ya Indonesia ilithibitisha kukamilika kwa mradi wa tarjuma ya Qur’ani Tukufu katika Kicirebon.

Lugha ya Cirebon ni lugha ya wenyeji nchini Indonesia inayohusiana na lahaja za Javanese na Banyumasan.
Ahmed Yani, ambaye aliongoza mradi wa kutafsiri, alisema tarjuma hiyo inalenga kukuza uelewa wa Qur’ani miongoni mwa wanaozungumza lugha hiyo.
Pia itasaidia kuhifadhi lugha hiyo, ambayo ni nembo ya kitamaduni ya eneo hilo, ambalo linajumuisha Cirebon, mji wa bandari kwenye pwani ya kaskazini ya kisiwa cha Java cha Indonesia, alibainisha.
Mradi wa tarjuma hiyo ulioanza mwaka wa 2020 ulihusisha timu ya watafsiri, alisema.
Timu hiyo pia ilijumuisha wataalamu wa Qur'ani pamoja na wasomi na wataalamu wa utamaduni wa Kicirebon, Yani aliongeza.
Muhammad Isam, afisa wa wizara ya masuala ya kidini ya Indonesia alishukuru jitihada za timu ya kutafsiri na kuthibitisha kwamba mojawapo ya malengo ya mradi huo ni kuhifadhi lugha ya Cirebon.
Alisema ni mojawapo ya lugha kumi za kienyeji za Indonesia ambazo zimejumuishwa katika mpango wa uwekaji tarakimu wa Qur'ani.

Habari zinazohusiana
captcha