IQNA

Wapalestina 45000 washiriki Sala ya Ijumaa Al Aqsa

21:03 - December 03, 2021
Habari ID: 3474635
TEHRAN (IQNA) – Maelfu ya Wapalestina wameshiriki katika Sala ya Ijumaa katika Msikiti wa Al Aqsa mjini Quds (Jerusalem) pamoja na kuwepo vizuizi vilivyokuwa vimewekwa na askari wa utawala wa Kizayuni wa Israel unaokalia ardhi hiyo ya Palestina kwa mabavu.

Kwa mujibu wa Kituo cha Habari cha Palestina, zaidi ya Wapalestina 45,000 wameshiriki katika Sala ya Ijumaa katika Msikiti wa Al Aqsa huku askari wa utawala dhalimu wa Israel wakiwa wamesambaza askari katika kila kona ya msikiti huo.

Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan walianza kuwasili katika Msikiti wa Al Aqsa mapema Ijumaa.

Hatibu wa Msikiti wa Al Aqsa Sheikh  Mohammed Sarandah. Amewapa bishara njema Wapalestina ambao wako katika mstari wa mbele kuuhami Msikiti wa Al Aqsa kuwa watapata ujira wao siku ya qiyama. Aidha amewapongeza Wapalestina ambao daima hujitokeza katika Msikiti wa al Aqsa.

Askari wa utawala wa Kizayuni wa Israel waliwazuia Wapalestina wengi kufika katika Msikiti wa Al Aqsa wakati wa Sala ya Ijumaa.

Msikiti wa Al Aqsa umegeuzwa kuwa eneo la kutamba na kujifaragua askari wa utawala haramu wa Israel na walowezi wa Kizayuni wanaochukua hatua zinazolenga kuubadilisha utambulisho wa Kiislamu na Kikristo wa mji wa Quds (Jerusalem) na badala yake kuufanya kuwa na nembo za Uzayuni.

Utawala wa Kizayuni unachukua hatua hizo za kibeberu kuhusiana na mji wa Baitul Muqaddas na msikiti wa Al Aqsa wakati Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO lilipitisha azimio mwaka 2016 lililopinga kuwepo uhusiano wowote wa kihistoria, kidini au kiutamaduni kati ya Mayahudi na maeneo matakatifu ya mji wa Quds na hasa msikiti wa Al Aqsa na kusisitiza kuwa, msikiti huo ni mahala patakatifu kwa Waislamu.

Mji wa Quds ulipo msikiti wa Al Aqsa ambao ni kibla cha kwanza cha Waislamu ni sehemu isiyotenganika na ardhi ya Palestina na moja ya maeneo matatu muhimu zaidi matakatifu ya Kiislamu.

/4018106

captcha