IQNA

Jinai za Israel

Wanajeshi wa Israel wazuia waumini kuingia Msikiti wa Al-Aqsa kwa Ijumaa ya tatu mfululizo

20:38 - October 27, 2023
Habari ID: 3477795
AL-QUDS (IQNA) - Vikosi vya Israel vimewabana waumini wa Kiislamu wa Kipalestina katika kitongoji cha Wadi Al-Joz mjini Al Quds (Jerusalem), na kuwazuia kufika Msikiti wa Al-Aqsa kwa ajili ya Sala ya Ijumaa ya kila wiki.

Mashuhuda waliripoti kuwa wanajeshi wa utawala dhalimu wa Israel walifyatua risasi za chuma zilizofunikwa kwa plastiki, mabomu ya machozi yenye sumu, na kutumia mizinga ya maji kuwashambulia waumini hao, wakiwafuata na kuwashambulia kimwili baadhi yao katika vurugu hizo.
Ni wachache tu waliofanikiwa kufika katika Msikiti wa Al-Aqsa kuswali Sala ya Ijumaa, kwani utawala ghasibu na wa kikoloni wa Israel ulitumia askari wake katili kuwazuia waumini kuingia katika eneo hilo takatifu.
Hii ni Ijumaa ya tatu mfululizo ambapo waumini wamekataliwa kuingia katika eneo la Msikiti wa Al-Aqsa. Kizuizi hiki kinachoendelea kimewalazimu kutekeleza sala zao katika mitaa ya jirani ya Wadi Al-Joz, ambayo ni karibu na Jiji la Kale la Quds Tukufu ambapo msikiti huo uko.

/3485756

 

Habari zinazohusiana
captcha