IQNA

UNESCO yatakiwa ichunguze uchimbuaji unaofanywa na Israel mjini Quds

22:56 - December 05, 2021
Habari ID: 3474644
TEHRAN (IQNA)- Maafisa wa Palestina wametaka Shirika la Umoja wa Mtaifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) lianzishe uchunguzi kuhusu uchimbuaji unaofanywa kinyume cha sheria na Israel katika mji wa Quds (Jerusalem).

Ahmed Al Ruwaidi, mshauri wa Mamlaka ya Palestina mjini Quds amesema tayari wameshawasilisha ombi kwa UNESCO wakitaka uchunguzi ufanyike.

Amesema kumeshuhudiwa maparomoko ya ardhi katika Eneo la Kale la Mji wa Quds na hivyo ametoa wito kwa UNESCO kutekeleza majukumu yake kuchunguza yanayofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Aidha ametahadharisha kuwa uchimbuaji huo wa chini ya ardhi sasa umefika katika Msikiti wa Al Aqsa na kuna nyufa ambazo zimeanza kuonekana katika nyumba za karibu kutokana na vitendo hivyo vya Wazayuni.

Utawala wa Kizayuni unachukua hatua hizo za kibeberu kuhusiana na mji wa Quds na msikiti wa Al Aqsa wakati Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO lilipitisha azimio mwaka 2016 lililopinga kuwepo uhusiano wowote wa kihistoria, kidini au kiutamaduni kati ya Mayahudi na maeneo matakatifu ya mji wa Quds na hasa msikiti wa Al Aqsa na kusisitiza kuwa, msikiti huo ni mahala patakatifu kwa Waislamu.

Mji wa Quds ulipo msikiti wa Al Aqsa ambao ni kibla cha kwanza cha Waislamu ni sehemu isiyotenganika na ardhi ya Palestina na moja ya maeneo matatu muhimu zaidi matakatifu ya Kiislamu.

4018501

Kishikizo: aqsa ، msikiti ، wazayuni ، quds ، palestina
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha