Akizungumza na IQNA Jumatano, Mikail Baqeri, mkurugenzi mkuu wa Qur’ani Etrat na Sala katika Wizara ya Elimu ya Iran amesema timu ya iran inajumuisha timbu mbili za wavulana na wasichana ambazo zitashiriki katika kategoria za kuhifadhi na kusoma Qur’ani.
Mchujo wa kuchagua wawakilishi wa Iran ulianza mwezi moja uliopita na majaji wamekuwa wakiwasikiliza washiriki kwa njia ya intaneti.
Mashindano hayo ya kimatiafa ya Qur’ani ya wanafunzi wa shule hufanyika mara moja kila miaka miwili nchini Iran. Mashindano ya awamu hii yanatazamiwa kufanyika baina ya Februari na Machi 2022 sambamba na mashindano ya kimataifa ya Qur’ani ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Baqeri anasema mazingira yakiruhusu, fainali ya mashindano hayo itafanyika hapa mjini Tehran kwa kushiriki ana kwa ana washindani.