IQNA

Ongezeko la chuki dhidi ya Uislamu barani Ulaya

19:17 - December 31, 2021
Habari ID: 3474746
TEHRAN (IQNA)- Ripoti mpya inaonyesha kuwa kumekuwepo na ongezeko kubwa la chuki dhidi ya Uislamu au Islamophobia barani Ulaya.

Hayo ni kwa mujibu wa riopoti mpya iliyochapishwa Jumatano yenye kurasa 886  yenye anuani ya ‘Chuki Dhidi ya Uislamu Ulaya Mwaka 2020’ ambayo imhaririwa kwa pamoja na  Enes Bayrakli, mhadhiri wa uhusiano wa kimataifa katika Chuo Kikuu cha Uturuki-Ujerumani mjini Istanbul na Farid Hafez, mtaalamu wa siasa katika Chuo Kikuu cha Georgetown.

Katika ripoti hiyo, ambayo imekuwa ikichapishwa kila mwaka tokea 2015, watafiti hao wawili wameandika: “Kwa kuangazia miaka sita iliyopita, wataalamu wengi wanaafikiana kuwa, sit u kuwa chuki dhidi ya Uislamu imeongezeka bali sasa imezidi kuwa mbaya.”

Aidha watafiti hao wanasema hali ni mbaya zaidi Ufaransa na Austria ambako serikali  za nchi hizo zimetunga sheria za kuwakandamiza Waislamu kwa kisingizo cha kupambana na ugaidi.

Kwa kuzingatia kuwa uchaguzi wa Ufaransa utafanyika Aprili 2021, wanasiasa nchini humo wanajaribu kuvutia kura za wapiga kura wa mrengo wa kulia kwa kueneza chuki dhidi ya Uislamu. Kwa msingi huo hali ya Waislamu inatazamiwa kuwa mbaya zaidi wakati huu wa kkukaribia uchaguzi mkuu nchini humo.

Ufaransa ina idadi kubwa zaidi ya Waislamu barani Ulaya. Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2016, kuna zaidi ya Waislamu milioni 5.7 Ufaransa ambao ni takribani asilimia 8.8 ya watu wote nchini humo.

3477163

captcha