IQNA

Misikiti 800 Ujerumani imelengwa na wenye chuki katika muda wa miaka minane

13:06 - June 11, 2022
Habari ID: 3475364
TEHRAN (IQNA) – Zaidi ya misikiti 800 nchini Ujerumani ililengwa kwa vitisho au ilishambuliwa na wenye chuki dhidi ya Uislamu kuanzia 2014 hadi 2022.

Brandeilig, mpango wa shirika la kutetea haki za binadamu la FAIR International, ilisema katika ripoti yake Ijumaa kwamba ilirekodi karibu matukio 840 ya mashambulizi, uharibifu na vitisho kati ya 2014 na 2022.

Hatahivyo kesi nyingi hazijachunguzwa ipasavyo. Uchambuzi wa kina wa uhalifu huo wa mwaka wa 2018 ulibaini kuwa wahalifu hawakujulikana katika mashambulizi mengi, na hivyo kuchochea mashambulizi zaidi dhidi ya maeneo ya ibada ya Kiislamu yanayofanywa na Wanazi mamboleo au watu wenye itikadi kali za mrengo wa kushoto na wenye chuki dhidi ya Uislamu.

Kati ya mashambulio 120 yaliyorekodiwa dhidi ya misikiti mnamo 2018, ni katika visa tisa tu ndio walioweza kutambuliwa.

"Kiwango hiki ni sababu ya wasiwasi," wataalam wa Brandeilig walisisitiza, wakisema kwamba katika angalau kesi 20, ambazo zilijumuisha uchomaji moto, washukiwa waliokusudia kusababisha kifo au madhara makubwa ya kimwili.

Brandeilig ilianzisha kituo cha kwanza cha kuripoti Ujerumani kwa mashambulizi dhidi ya misikiti - na wataalam wake wanasema "karibu matukio yote yaliyoripotiwa hayakuweza kutatuliwa."

Ujerumani, nchi yenye zaidi ya watu milioni 83, ina idadi ya pili ya Waislamu katika Ulaya Magharibi baada ya Ufaransa.

3479253

captcha