IQNA

Mkuu wa Al Azhar asisitiza kuhusu maelewano ya kidini

18:41 - January 05, 2022
Habari ID: 3474770
TEHRAN (IQNA)- Shekhe Mkuu wa Kituo cha Kiislamu cha Al Azhar nchini Misri amesema chimbuko la dini za mbinguni ni moja na wanadamu wote wana udugu.

Sheikh Ahmed el Tayeb ameyasema hayo Jumanne wakati alipokutana na kiongozi wa Kikristo Misri Papa Tawadros II wa Alexandria.

Papa Tawadros II, wa  dhehebu la Kopti (Khufti),   alimkaribisha Sheikh Mkuu wa Al Azhar katika makao yake na kuseme mikutano kama hivyo inaeneza maelewano na hilo ni kwa maslahi ya jamii nzima.

Aidha amesisitiza umuhimu wa kuwepo amani katika familia, jamii na dunia nzima kwa ujumla.

Kwa upande wake Sheikh El Tayeb amempongeza kiongozi huyo wa Kikristo kwa mnasaba wa kuwadia mwaka mpya.

Aidha amesisitiza kuhusu umuhimu wa amani na kuongeza kuwa, amani ni nukta inayosisitizwa na Waislamu katika Sala.

Mkuu wa Kituo cha Kiislamu cha Al Azhar aidha amesisitiza kuhusu chimbuko la pamoja la dini zote.

Misri ni nchi iliyo Afrika Kaskazini ambapo idadi ya watu wake inakadiriwa kuwa milioni 100 ambapo asilimia 90 ya watu wake ni Waislamu. Nchi hiyo pia ina kubwa ya Wakristo ambapo dhehebu la Kopti ndilo kubwa zaidi. Inakadiriwa kuwa kuna Wakopti karibu milioni saba nchini Misri na hivyo kuifanya Misri kuwa nchi yenye idadi kubwa zaidi ya Wakristo miongoni mwa nchi zote za Kiarabu.

4026387  

captcha