IQNA

Mazungumzo baina ya dini

Mufti wa Kazakhstan asifu Iran kwa Kukuza mazungumzo ya dini mbalimbali

22:48 - September 15, 2022
Habari ID: 3475789
TEHRAN (IQNA) - Mufti Mkuu wa Kazakhstan Sheikh Nauryzbay Kazhy Taganuly amepongeza nafasi ya kimkakati ya Iran katika kukuza mazungumzo kati ya dini mbali mbali.

Akizungumza katika kikao na ujumbe wa Iran mjini Nur-Sultan, Sheikh Taganuly pia amesema kuwa, watu wa nchi hiyo ya Asia ya Kati wana heshima ya pekee kwa watu wa Iran.

Ujumbe wa Iran ukiongozwa na Mkuu wa Shirika la Utamaduni na Uhusiano wa Kiislamu Hujjatul Islam Mohammad Mehdi Imanipour, umesafiri hadi Kazakhstan kuhudhuria Kongamano la 7 la Viongozi wa Dini za Dunia.

Ameongeza kuwa ziara ya hivi majuzi ya rais wa Kazakhstan nchini Iran itabadilika na kuwa hatua ya kihistoria katika uhusiano kati ya mataifa hayo mawili.

Katika mkutano huo Hujjatul Islam Imanipour alisisitiza haja ya kuendeleza ushirikiano wa pamoja kati ya Iran na Kazakhstan katika nyanja za kitamaduni na kidini.

Pia, mjumbe mwingine wa ujumbe huo, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu Hujjatul Islam Hamid Shahriari, alimwalika Sheikh Taganuly kuhudhuria Mkutano ujao wa Kimataifa wa Umoja wa Kiislamu nchini Iran.

Kongamano la VII la Viongozi wa Dini za Ulimwengu na Dini za Kimila lilianza katika mji wa Nur-Sultan mnamo Septemba 13 na limehitimishwa leo.

Zaidi ya viongozi140 wa kidini, kitamaduni na wasomi wengine kutoka nchi 60 wamehudhuria hafla hiyo ya kimataifa.

Viongozi wa kidini waliohudhuria kikao hicho ni pamoja na Kiongozi wa Kanisa Katoliki Papa Francis, Imam Mkuu wa  Kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar cha Misri,  Sheikh Ahmed Al-Tayyeb,  Kasisi Mkuu wa Moscow na Russia, Mwenyekiti wa Kurugenzi ya Masuala ya Kidini ya Uturuki, na Mwenyekiti wa Bodi ya Waislamu wa Caucasus.

Kongamano hilo hufanyika katika jiji hilo la Kazakhstan kila baada ya miaka mitatu.

4085746

captcha