IQNA

21:01 - January 07, 2022
Habari ID: 3474779

Mwanzilishi wa Darul Hadith Nigeria aaga dunia

TEHRAN (IQNA)- Mwanazuoni maarufu wa Nigeria na muasisi wa Taasisi ya Darul Hadith ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 79.

Mwanzilishi wa Darul Hadith Nigeria aaga dunia

Sheikh Ahmad Ibrahim Bamba amefariki Ijumaa asubuhi mjini Kano kaskazini mwa Nigeria.

Kwa mujibu wa taarifa, mwendazake alipoteza maisha baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Kifo cha Sheikh Ibrahim Bamba kimetangazwa na mmoja wa wanae, Ahmad Muhammad Ahmad.

Sheikh Bamba aliwahi kuwa mhadhiri wa lugha ya Kiarabu katika Chuo Kikuu cha Bayero Kano kabla ya kujiuzulu na kuanzisha  chuo chake cha Kiislamu alichokipatia jina la  Taasisi ya Darul Hadith.

 4026956

captcha