Baraza hilo limetoa wito pia kwa serikali ya Taliban kuwarejeshea vijana wa kamati za kulinda misikiti. Wamesema kuwa wana wasi wasi mkubwa kuwa awana ulinzi baada ya maafisa wa utawala wa Taliban kuwapokonya vijana sialaha.
Halikadhalika baraza hilo limesema tokea utawala wa Taliban uingie madarakani mwezi Agosti, kumekuwepo na hujuma nyingi dhidi ya misikiti ambazo zimetekelezwa na ISIS.
Mwezi uliopita zaidi ya waumini sitini waliuawa shahidi baada ya kundi la kigaidi la ISIS kutekeleza hujuma dhidi ya msikiti wa Mashia mjini Kandahar wakati wa Sala ya Ijumaa. Hujuma hiyo ilikuja wiki mbili tu baada ya magaidi hao hao wa ISIS kushambulia msikiti katika mji wa Kunduz na kuua shahidi waumini zaidi ya 100. Mamia ya watu walijeruhiwa katika hujuma hizo mbili.