IQNA

21:41 - January 24, 2022
Habari ID: 3474848
TEHRAN (IQNA)-Idara ya Masuala ya Kidini Uturuki (Diyanet) imetangaza mpango wa kuongeza idadi ya waliohifadhi Qur’ani Tukufu nchini humo.

Mkuu wa Diyanet, Sheikh Ali Erbas amesema hivi sasa watu 200,000 kote Uturuki wameweza kutambuliwa rasmi kuwa waliohifadhi Qur’ani Tukufu kikamilifu na hivi sasa kuna waumini wengine 80,000 walio katika darsa za kuhifadhi Qur’ani Tukufu.

Sheikh Erbas amesema lengo la Diyanet ni kutoa mafunzo zaidi kwa wanotaka kuhifadhi Qur’ani Tukufu kikamilifu ili idadi hiyo ifike 840,000 au asilimia moja ya watu wote wa Uturuki.

Mkuu wa Diyanet amesema mafunzo ya kuhifadhi Qur’ani Tukufu yanatolewa kwa wanaume na wanawake walio katika makundi yote ya umri. Mbali na darsa za kuhifadhi Qur’ani Tukufu wanapata pia mafunzo ya tafsiri ya Kitabu hicho kitakatifu.

4030835

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* captcha: