IQNA

Wavamizi waendeleza jinai Yemen, Jeshi la Yemen lalipiza kisasi kwa kushambulia UAE

10:23 - January 31, 2022
Habari ID: 3474871
TEHRAN (IQNA)- Milipuko kadhaa mikubwa imesikika katika anga ya Umoja wa Falme za Kiarabu punde tu baada ya majeshi ya Yemen kutangaza oparesheni kubwa ya ulipizaji kisasi dhidi ya vituo muhimu vya kiuchumi vya nchi hiyo.

Vyombo kadhaa vya habari vimeripoti kuwa milipuko ya makombora imesikika mapema Jumatatu asubuhi katika mji mkuu wa UAE, Abu Dhabi katika kile kinachoonkena na oparesheni ya ulipizaji kisasi wa majeshi ya Yemen kufuatia jinai za UAE dhidi ya Wayemen. Televisheni ya Al Masira mapema ilikuwa imenukuu msemaji wa Jeshi la Yemen Yahya Saree akisema, 'majeshi yatatangaza oparesheni kubwa ya kijeshi katika kitovu cha UAE"

Tovuti ya alkhabaralyemeni.net imesema oparesheni hiyo ilikuwa inalenga maeneo 50 nyeti kote Umoja wa Falme za Kiarabu.

Shambulizi hilo la makombora la ulipizaji kisasi la Wayemen limetekelezwa huku rais wa utawala haramu wa Israel Issac Herzog akiwa safarini Abu Dhabi. Shirika la Habari la Reuters limeandika kuwa Herzog ataendelea na safari yake hiyo. Hatahivyo gazeti la Kizayuni la Yedioth Ahronoth limeripoti kuwa mashirika ya kijasusi ya Israel yamemtaka Herzog aondoke UAE mara moja.

Inafaa kuashiria kuwa, Saudia ikishirikiana na UAE na kwa himaya ya Mareakni na utawala haramu wa Israel na madola mengine ya magharibi ilianzisha mashambulizi dhidi ya Yemen mwishoni mwa mwezi Machi 2015 kwa lengo la kuiondoa madarakani Harakati ya Ansarullah na kumrejesha usukani Abdrabbuh Mansour Hadi, rais wa zamani wa nchi hiyo aliyejiuzulu na kukimbilia Riyadh.

Vita vilivyoanzishwa  na Saudi Arabia na washirika wake dhidi ya Yemen na kuendelea hadi sasa vimeshapelekea mamia ya maelfu ya watu wasio na hatia kupoteza maisha, mbali na kuwaacha mamilioni wakiwa hawana pa kuishi. Aidha vita hivyo vimesababisha matatizo mengi ya ukosefu wa chakula, matibabu na elimu kwa watu wa Yemen.

Katika kulipiza kisasi jinai hizo, Jeshi la Yemen hutekeleza mashambulizi ya mara kwa mara dhidi ya maeneo ya kistratijia ya Saudi Arabia na UAE.

4032579/

captcha