IQNA

Ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu

Kiongozi Muadhamu azuru Haram ya Imam Khomeini MA na maziara ya Mashahidi

11:30 - January 31, 2022
Habari ID: 3474873
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapunduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei mapema leo asubuhi amefanya ziara katika Haram toharifu ya Imam Khomeini MA, mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu na maziara ya Mashahidi katika Makaburi ya Behesht Zahra SA kusini mwa Tehran.

Katika wakati huu wa kukaribia maadhimisho ya miaka 43 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Kiongozi Muadhamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei mapema leo asubuhi amefanya ziara katika Haram toharifu ya Imam Khomeini MA, mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu na mbali na kuswali katika Haram hiyo na kusoma Qur'ani, amemkumbuka na kumuenzi Imamu huyo wa taifa la Iran.

Vile vile Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amezuru maziara ya mashahidi  wakubwa kama vile mashahidi Beheshti, Rajai, Bahonar na mashahidi wengine wa tukio la tarehe 7 Tir na kuwaombea dua za kheri ili Mwenyezi Mungu awapandishe daraja za juu waja wake hao wema.

Baada ya hapo Ayatullah Khamenei amefanya ziara katika maziara ya mashahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, wa vita vya kujihami kutakatifu, mashahidi wa kulinda Haram na mashahidi wa Hija na kumuomba Allah azipe utulivu na kila la kheri roho za wapigania haki hao.

Itakumbukwa kuwa siku ya Alkhamisi ya Februari 1, 1979, Imam Khomeini (MA) alirejea nchini Iran kutoka uhamishoni kwa muda wa miaka 15, na kurejea kwake huko kulitia nguvu harakati za mapinduzi ya wananchi wa Iran yaliyoung'oa madaraka utawala wa kidikteta wa Shah, Februari 11, 1979.

Siku hizo kumi za baina ya kurejea nchini Iran Imam Khomeini (MA) hadi kupatikana ushindi kamili wa Mapinduzi ya Kiislamu ni maarufu kwa jina la Dahe Fajr yaani Alfajiri Kumi na huadhimishwa kila mwaka. Sherehe hizo hufikia kileleni Februari 11, siku ambayo ni maarufu kwa jina la Bahman 22 ambayo wananchi wa Iran husherehekea

/4032586

captcha