IQNA

Salamu za Spika wa Bunge la Lebanon wakati wa maadhimisho ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu

21:22 - February 10, 2022
Habari ID: 3474913
TEHRAN (IQNA)- Nabih Berri, Spika wa Bunge la Lebanon amemtumia ujumbe Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Seyed Ali Khamenei ambapo amempongeza kwa kuadhimisha mwaka wa 43 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Katika ujumbe wake, Berri alisema miaka 43 imepita tangu mwanzo wa uthabiti, utulivu, ubora, uimara na nguvu nchini Iran.

Haya yote yamepatikana kutokana na ushindi wa mapinduzi yaliyoongozwa na hayati mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu Imam Khomeini (Mwenyezi Mungu Amrehemu) ambayo yaliendelea "chini ya uongozi wako wa busara", aliongeza katika ujumbe huo.

Berri amempongeza Ayatullah Khamenei na taifa la Iran kwa mnasaba huo na kumuombea afya Kiongozi na uwezo, maendeleo na ushindi kwa Jamhuri ya Kiislamu na wananchi na serikali ya Iran.

Kila mwaka, mamilioni ya Wairani kote nchini huadhimisha siku kumi za kumbukumbu ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya mwaka 1979 yaliyokomesha utawala wa kiimla na kifalme wa ukoo katili wa Pahlavi uliokuwa unaungwa mkono na Marekani nchini humo.

Siku ya kurejea kwa Imam Khomeini nchini Iran (Februari 1 mwaka huu) ni mwanzo wa Siku Kumi za Fajr (Alfajiri), ambazo hufikia kilele kwa mikusanyiko ya maadhimisho ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu tarehe 11 Februari.

Taifa la Iran liliupindua utawala huo dhalimu wa Pahlavi uliopata himaya ya Marekani miaka 43 iliyopita, na hivyo kuhitimisha miaka 2,500 ya utawala wa kifalme nchini humo.

Mapinduzi ya Kiislamu yaliyoongozwa na hayati Imam Khomeini yalianzisha mfumo mpya wa kisiasa unaozingatia maadili na demokrasia ya Kiislamu.

4035308

 

captcha