IQNA

Rais wa Iran akutana na mabalozi wa kigeni katika maadhimisho ya Mapinduzi ya Kiislamu

19:58 - February 10, 2022
Habari ID: 3474911
TEHRAN (IQNA)- Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kikao na mabalozi wa nchi za nje hapa mjini Tehran kwa mnasaba wa kukumbuka ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa: "Taifa la Iran limesimama imara katika misingi ya itikadi za mapinduzi yake."

"Mapinduzi ya Kiislamu ni matokeo ya imani ya kina ya wananchi kwa misingi na thamani za juu za Uislamu, kutafuta uhuru, kutafuta haki na uongozi wenye busara," ameongeza Rais wa Iran Seyyed Ebrahim Raisi leo (Alhamisi) mjini Tehran katika mkutano na mabalozi wa kigeni.

Huku akiashiria kwamba madola mengi makubwa ya kibeberu yanajaribu kuizuia Iran kuwa katika nafasi ambayo inastahiki kuwa nayo,  Rais amebainisha: Sera ya mambo ya nje ya serikali ya 13 inatokana na misingi na maadili yaliyomo ndani ya Katiba na pia kwa kuzingatia miongozo ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kuhusu vipaumbele vitatu vya "maingiliano ya juu kabisa na nchi jirani, na washirika", "kuzingatia mashirika ya kikanda na kimataifa," na "maendeleo ya diplomasia ya kiuchumi."

Raisi amesema: Iran pamoja na mwambao wake mkubwa wa bahari na uwezo wa juu sana hususan katika nyanja za usafiri, nishati, biashara, kilimo, viwanda na teknolojia ina nia ya kuunda na kuendeleza nafasi mpya ya ushirikiano wa manufaa na uhusiano na nchi jirani na rafiki.

Rais Raisi amesema ingawa suala la kuwa na uhusiano na nchi jirani na za bara Asia linapewa kipaumbele na serikali yake lakini pia kuna jitihada  maalumu zinazofanyika kwa ajili ya kuimarisha uhusiano na nchi za Afrika, Amerika ya Latini na Ulaya.

134507

captcha