IQNA

Maonyesho ya Hijabu yafanyika Tanzania

17:22 - February 06, 2022
Habari ID: 3474897
TEHRAN (IQNA)- Kituo cha Utamaduni cha Iran nchini Tanzania kimeandaa maonyesho ya Hijabu kwa ushirikiano na Taasisi ya Pink Hijab.

Maonyesho hayo yalifanyika katika kuadhimisha Siku ya Hijabu Duniani, ambayo huadhimishwa duniani kote tarehe 1 Februari kila mwaka.

Sherehe za ufunguzi huo zilihudhuriwa na mabalozi wa Iran na Uturuki nchini Tanzania, Mkuu wa wanawake wa Kiislamu Tanzania Bara chini ya mwamvuli wa Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata) Shamim Khan, na Waziri wa Nchi Afisi ya Rais - Kazi, Uchumi na Uwekezaji Mhe. Mudrik Ramadhan Soraga .

Katika hotuba yake, mkurugenzi wa Taasisi ya Pink Hijab Khadija Omari alieleza kuhusu juhudi za taasisi hiyo kukuza nafasi ya wanawake katika jamii.

Mzungumzaji mwingine alikuwa ni Bw. Morteza Pirani, Mwambata wa Utamaduni wa Iran nchini Tanzania, ambaye alisema maonyesho hayo yanalenga kuwafahamisha watu mavazi ya wanawake wa Kiislamu katika nchi mbalimbali.

Vile vile ameashiria kumbukumbu ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya 1979 na kuashiria mafanikio ya wanawake tangu ushindi wa mapinduzi hayo.

Waziri Soraga pia alihutubia tukio hilo, akisema maonyesho hayo ni ukumbi wa mazungumzo na kubadilishana mawazo kuhusu kuboresha sera za vazi la staha la Hijabu.

Siku ya Hijabu Duniani ni tukio la kila mwaka lililoanzishwa na Nazma Khan mwaka wa 2013, na huadhimishwa Februari 1 kila mwaka katika nchi 140 duniani kote.

Madhumuni yake ni kuwahimiza wanawake wa dini zote na asili zote kuvaa na kujionea hijabu kwa siku moja na kuelimisha na kueneza ufahamu juu ya kwa nini hijabu inavaliwa.

 

4034114

captcha