Nasr al-Shammari aliyasema hayo kongamano la kimataifa la “Mazungumzo ya Mapinduzi ya Kiislamu; Mbinu ya Mapambano (Muqawama) Duniani.”
Kongamano hilo limeandaliwa kwa njia ya intaneti na Shirika la Habari za Qur'ani Tukufu la Kimataifa (IQNA) kwa mnasaba wa kuadhimisha mwaka wa 43 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
.Al-Shammari amesisitiza kuwa, baada ya Vita Vikuu vya Pili vya Dunia, ni Jamhuri ya Kiislamu pekee iliyoweza kusimama dhidi ya Marekani, akimaanisha mapigo mawili ya hadharani ya Iran dhidi ya Marekani, nayo ni kutekwa kwa "Pango la Majasusi" (ubalozi wa zamani wa Marekani mjini Tehran ) na mashambulizi dhidi ya kituo cha Jeshi la Marekani cha . Ayn al-Asad nchini Iraq.
Ameyataja mapambazuko ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran kuwa ni “mwisho wa karne nyingi za dhulma na giza ambalo, kama jua linalowaka, huangazia wakati wetu na zama zinazofuata.”
Al-Shammari aliendelea kwa kuusifu uongozi wa Imam Khomeini-Mwenyezi Mungu Amrehemu- akisema: “Tangu siku za mwanzo za ushindi wa mapinduzi haya yenye baraka, wasi wasi wa dunia nzima ulikuwa ni kufahamu asili ya mapinduzi haya. Hata hivyo, sauti nzuri ilipaza sauti kwamba ‘haya [mapinduzi] si ya Mashariki wala si ya Magharibi, bali ni mapinduzi ya Kiislamu ambayo yamechipuka kutoka kwenye moyo wa Uislamu na mafundisho na kanuni zake.’”
Ameitaja nguvu ya Mapinduzi ya Kiislamu kuwa ni "damu ya vijana waumini na wa Kiislamu" na kuongeza kuwa, "Siasa ya mapinduzi haya ni Uislamu na misingi yake ni nchi za Kiislamu. Adui wake pia ni mamlaka zenye kiburi za ulimwengu, popote ambapo pembe zao mbaya zimepenya.”
Akikumbuka ukweli kwamba katika kipindi cha kuelekea Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, dunia iligawanyika baina ya kambi mbili - Ukomunisti wa Kisoshalisti na Magharibi ya Kibepari, msemaji wa al-Nujaba ameongeza kuwa: "Kambi zote mbili ziliuona ulimwengu wa Kiislamu kuwa ni adui ambaye alipaswa kudhoofishwa na kudhibitiwa."
Al-Shammari, akitoa mifano ya uvamizi wa kidhalimu wa kambi hizo dhidi ya maeneo mbali mbali ya dunia, alisema, “Wakati huo, hakuna hata mmoja aliyethubutu kupinga kambi hizo. Lakini mwanzoni mwa mapinduzi hayo yenye baraka, mataifa ya ulimwengu yalifahamu misimiati mipya ya kimapinduzi kama vile ‘mapambano ya Kiislamu au muqawama’ na ‘ukakamavu’ na ‘makabiliano na madola ya kiistikbari duniani.’”
Amebainisha kuhusiana na suala hilo kuwa, “Dunia pia iliona vijana wenye sura ya watu wema waliofunga ubalozi wa utawala wa Kizayuni na kupandisha bendera ya taifa la Palestina mjini Tehran. Hili lilitokea baada ya serikali za Kiarabu kusalimu amri na kulegeza misimamo ili kuachana na kadhia ya Palestina."
Msemaji rasmi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya al-Nujabaa ya Iraq alitaja kutekwa kwa "Pango la Majasusi" (ubalozi wa Marekani mjini Tehran) na akasema, "Ulimwengu haujawahi kuona hatua kama hii iliyojaa baraka. Kwa namna ambayo midomo ya watu wajasiri zaidi ilibaki wazi kwa mshangao kwa sababu hawakufikiri kwamba nchi ingeweza kukabiliana na Marekani waziwazi katika ulimwengu wa baada ya Vita Kuu ya II.
Al-Shammari aliongeza: "Baada ya pigo hili la kwanza, pigo jingine la hadharani lazima likumbukwe, ambalo pia lilitoka kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran - ambapo, baada ya jinai kubwa ya Trump na mauaji ya makamanda waliouawa shahidi (Haj Qasem Soleimani na Haj Abu Mahdi). al-Muhandis), Jeshi la Iran lililengwa kwa uwazi ngome ya Marekani huko Ayn al-Asad nchini Iraq.
Katika sehemu nyingine ya hotuba yake amesisitiza kuwa: “Leo sote tunaona na tunajua kwamba popote pale panapopigwa vita dhidi ya madola kiistikbari ya dunia na utawala wa Kizayuni bila shaka kuna mikono yenye baraka ya Jamhuri ya Kiislamu na moyo wa mwanzilishi wake mkuu, pamoja na idhini ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu (Mwenyezi Mungu amhifadhi).”
Kwa kumalizia, mjumbe wa ngazi za juu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya al-Nujabaa ya Iraq alitoa pongezi kwa hayati Imam Khomeini, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei na mashahidi wa Uislamu, na kusema, “Katika Mapambano ya Kiislamu, tuna deni kubwa kwa Mapinduzi ya Kiislamu kutokana na kila tulichonacho, ikiwa ni pamoja na kuchukua msimamo, silaha zetu na nguvu za mioyo yetu mbele ya madola yenye kiburi. Haya ni Mapinduzi ya Kiislamu ambayo shahidi Sayyid Muhammad-Baqir al-Sadr aliyataja kuwa ni ‘ndoto ya Mitume’ na akiwahutubua Waislamu alisisitiza haja ya ‘kujitosa kikamilifu katika mapinduzi haya na mwanzilishi wake, Imam Khomeini.’”