IQNA

Rais wa Iran apokea vitambulisho vya balozi wa Palestina, asema

Umoja wa makundi na mirengo yote ya Palestina ni siri ya kuwashinda Wazayuni

19:14 - February 08, 2022
Habari ID: 3474907
TEHRAN (IQNA)- Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amepokea vitambulisho vya balozi mpya wa Palestina mjini Tehran na kusisitiza kuwa: "Umoja na mashikamano wa makundi na mirengo yote ya Palestina ni siri ya kupata ushindi katika mapambano dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel."

Rais Ibrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran akizungumza leo Jumanne baada ya kupokea vitambulisho vya Bi. Salam Zawawi, balozi mpya wa Palestina mjini Tehran amesema: "Harakati ya pamoja ya Wapalestina, hatimaye itapelekea kufikiwa lengo la ukombozi wa Quds (Jerusalem) Tukufu na hivyo hakupaswi kuwa na uvurugaji wowote wa mchakato huo."

Raisi ameongeza kuwa: "Kuwaunga mkono watu wa Palestina na kukombolewa Quds Tukufu ni kadhia nambari moja katika ulimwengu wa Kiislamu na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni muungaji mkono wa kweli wa watu wa Palestina na ukombozi wa Quds."

Rais wa Iran ameendelea kusema nchi na mataifa ya Kiislamu yanapaswa kuipatia kipaumbele kadhia ya Palestina na kuongeza kuwa: "Baadhi wameingizwa katika mchezo wa kisiasa katika kadhia ya Palestina na wanategemea mapatano na mikataba dhaifu na hivyo kupunguza kasi ya harakati ya kijihadi  ya Wapalestina lakini hawajazingatia kuwa waliotia saini nao mikataba hiyo kawaida huvunja ahadi zao."

Rais wa Raisi ameendelea kusema kuwa, ujumbe  ambao Wapalestina wanautuma kwa  utawala wa Kizayuni na waitifaki wake wa Kimagharibi ni kuwa taifa la Palestina litasimama kidete na litavuruga  mahesabu yao.

Aidha Rais wa Iran ameashiria hatua ya baadhi ya madola ya Kiarabu ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni na kusema, madola hayo yanapaswa kufahamu malalmiko ya Wapalestina wote kuhusu kadhia hii ni dalili wazi kuwa kitendo chao ni  uhaini. 

Kwa upande wake, balozi mpya wa Palestina mjini Tehran Salam Zawawi ameanza kwa kutuma salamu za kheri na fanaka kwa mnasaba wa kuwadia mwaka wa 43 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu na huku akiipongeza Iran kwa kuwaunga mkono Wapalestina amesema: "Ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ulikuwa ushindi mkubwa kwa mataifa ya Kiarabu na Kiislamu."  Aidha amesema hatua ya baadhi ya nchi za Kiarabu kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni ni sawa na kupuuza haki na malengo matukufu ya ukombozi wa Palestina. 

Aidha balozi mpya wa Palestina mjini Tehran amesema: "Nina matumaini kuwa, kwa kupatikana ushindi na kuundwa taifa huru la Palestina, mji wake mkuu ukiwa ni Quds Tukufu, tutaweza kusali katika Msiktii wa Al Aqsa katika sala itakayosalishwa na Ayatullah Khamenei."

/4034911

captcha