IQNA

Gharama za maisha zawahangaisha Waislamu wa Uingereza

22:07 - March 14, 2022
Habari ID: 3475042
TEHRAN (IQNA) – Huku Waislamu kote Uingereza wakihangaika kujikimu, Mfuko wa Kitaifa wa Zakat (NZF) umeripoti ongezeko la asilimia 90 la maombi ya mahitaji muhimu kama vile chakula na nguo ikilinganishwa na mwaka jana.

Takwimu kutoka NZF zinasema maombi ya usaidizi wa dharura yanatoka kwa familia, wakimbizi, wazazi wasio na wenzi wa ndoa na wengine wanaotatizika kulipia mahitaji ya msingi.

Na shirika la usaidizi linasema takwimu zao zinaonyesha kuwa 50% ya Waislamu wa Uingereza ambao tayari wanaishi katika umaskini wanaathirika zaidi na kuongezeka kwa gharama ya maisha magumu.

Waislamu walikuwa mojawapo ya makundi yaliyoathirika zaidi nchini Uingereza na janga la virusi vya corona, huku Sensa ya Waislamu ikiripoti kiwango cha umaskini mara 10 zaidi ya wastani wa kitaifa.

Sohail Yanif, Mtendaji Mkuu wa shirika hilo, alisema: “Tunaona viwango vya juu vya mahitaji kuliko wakati wowote katika historia yetu. Huku Ramadhani ikiwa inakaribia, tunategemea jamii ya Waislamu kutoa Zaka zao nchini Uingereza ili tuweze kukidhi mahitaji haya.

Taasisi ya Uchunguzi wa Fedha ilisema uwezekano wa athari za mzozo wa Ukraine kwenye mfumuko wa bei na fedha za umma zinaweza kumlazimisha waziri wa fedha kuchukua hatua atakapotoa taarifa yake ya majira ya kuchipua baadaye mwezi huu.

3478129

captcha