IQNA

Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani ya Saudia yamalizika

22:32 - April 21, 2022
Habari ID: 3475152
TEHRAN (IQNA)- Mashindano ya Qur’ani Tukufu na Adhana yajulikanayo kama Otr Elkalam ya Saudi Arabia yamemalizika katika mji wa Jeddah nchini humo.

Kwa mujibu wa taarifa washindi katika kategoria ya qiraa au kusoma Qur’ani Tukufu walikuwa ni Mustafa Maghrebi wa Morocco ambaye alipata nafasi ya kwanza akifuatiwa na  Muhammad Ayub Asef wa Uingereza, Muhammad Mujahid wa  Bahrain huku nafasi ya nne ikishikwa na Sayyid Jassem Mousavi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Mashindano hayo yalianza katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ambapo takribani washiriki 40,000 kutoka nchi 80 walishiriki katika mchujo wa mashindano hayo kwa kutuma klipu za qiraa yao ya aya za Qur’ani Tukufu au adhana katika mashindano hayo.

Katika kategoria ya adhana nafasi nafasi ya kwanza imeshikwa na Mohsen Kara wa Uturuki huku Albijan Celik wa Uturuki pia akishika nafasi ya pili huku nafasi za tatu na nne zikiwaendea waadhini kutoka Saudia.

Mamlaka ya Tamasha Saudia inasema ilitenga kiwango kikubwa zaidi cha zawadi katika mashindano ya Qur’ani duniani ambapo jumla ya zawadi zilizotolewa zina thamani ya dola milioni 3.2.

Mshindi wa kwanza katika qiraa ya Qur’ani Tukufu alipata zawadi ya dola milioni 1.3 na mshindi mwenye sauti bora zaidi ya adhana atapata zawadi ya dola laki 5.3. Fedha zilizosalia zimewaendea washindi wengine sita.

4051282

captcha