IQNA

Ustadh Mousavi wa Iran afika fainali ya mashindano ya Qur'ani Saudia + Video

17:29 - April 20, 2022
Habari ID: 3475147
TEHRAN (IQNA)- Qarii wa Qur'ani Tukufu kutoka Iran Sayyed Jassem Mousavi amefika katika fainali ya mashindano ya kimataifa ya Qur'ani nchini Saudi Arabia.

Wengine walioingia katika fainali ya mashindano hayo ni  Muhammad Mujahid wa Bahrain, Muhammad Ayub Asef wa Uingereza na Mustafa Maghrebi wa Morocco.

Kwa mujibu wa taarifa, takribani washiriki 40,000 kutoka nchi 80 walishiriki katika mchujo wa mashindano hayo kwa kutuma klipu za qiraa yao ya aya za Qur’ani Tukufu au adhana katika mashindano hayo yajulikanayo kama Otr Elkalam.

Baada ya mchujo hatimaye washiriki 36 walifika katika fainali. Miongoni mwa waliofika fainali ni wawakilishi wa Saudi Arabia, Iran, Misri, Iraq, Algeria, Uturuki, Morocco, Bahrain, Malaysia, Indonesia, Canada na Uingereza.

Mamlaka ya Tamasha Saudia imesema imetenga kiwango kikubwa zaidi cha zawadi katika mashindano ya Qur’ani duniani ambapo jumla ya zawadi zitakazotolewa zina thamani ya dola milioni 3.2.

Mshindi wa kwanza katika qiraa ya Qur’ani Tukufu atapata zawadi ya dola milioni 1.3 na mshindi mwenye sauti bora zaidi ya adhana atapata zawadi ya dola laki 5.3. Fedha zilizosalia zitawaendea washindi wengine sita.

Hii hapa chini klipu ya qiraa ya Ustadh Mousavi akisoma aya ya 206 ya Sura Al A'raf katika semi fainali za mashindano hayo.

 
captcha