IQNA

Mashindano ya Qur'ani Tukufu

TV ya Saudia yaanza kurusha hewani Mashindano ya Qur’ani na Adhana

14:07 - March 25, 2023
Habari ID: 3476756
TEHRAN (IQNA) – Televisheni ya MBC ya Saudi Arabia imeanza kutangaza mfululizo wa pili wa mashindano ya kimataifa ya usomaji wa Qur'ani Tukufu na Adhana.

Mashindano hayo yanaoitwa Harufu ya Usemi (Otr Elkalam) awai yalifanyika kwa njia ya intaneti ambapo washindani walituma video zao ambazo zilichunguzwa na jopo la majaji.

Washindani ambao walipita awamu tatu za kwanza sasa watasikilizwa na watazamaji wa kipindi cha MBC katika mwezi mtukufu wa Ramadhani ili kuwania zawadi bora.

Mashindano hayo yamekusudiwa kuufahamisha ulimwengu mzima juu ya uvumilivu na ustahimilivu wa Uislamu na vile vile uboreshaji wa tamaduni za Kiislamu na sauti nzuri za kusoma Qur’ani Tukufu na kuomba dua pamoja na kuwaunga mkono na kuwawezesha wenye ujuzi na wabunifu na kuwaenzi. kulingana na waandaaji.

Mamlaka ya Saudia imetenga zaidi ya zawadi za thamani ya SR12 milioni kwa washindi wa hafla hiyo, inayosemekana kuwa programu kubwa zaidi ya shindano ulimwenguni la aina yake.

Zawadi hizi zitasambazwa kwa washindi 20 wakuu katika kategoria za usomaji wa Qur’ani Tukufu na Adhana.

Zaidi ya washindani 50,000 kutoka nchi 165 walishiriki katika hatua ya kwanza. Walitoka nchi kama Morocco, Saudi Arabia, Marekani, Syria, Mauritania, Iran, Nigeria, Uturuki, Indonesia, Afghanistan, Yemen, Ethiopia, Pakistan, Lebanon, Libya, Misri, Umoja wa Falme za Kiarabu, Uingereza, Hispania, Ufaransa, na Bangladesh.

4129739

captcha